Mradi wa Veta Nala mbioni kukamilika

0
235

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 17 katika ujenzi wa awamu ya kwanza wa Chuo Cha Ufundi kinachojengwa Nala mkoani Dodoma ambacho kinatarajiwa kukamilika mwakani na kuleta mageuzi makubwa katika fani ya ufundi nchini.

Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo hicho ambapo amesema ujenzi huo unaenda sambamba na mapitio ya sera na mitaala ya elimu ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira Duniani

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi Mhandisi Aliki Nziku ameeleza hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo huku Mkurugenzi wa Ufundi Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Noel Mbonde akifafanua mafunzo ya fani za awali zitakazotolewa chuoni hapo