Mradi wa umeme wa Nyerere waneemesha maelfu ya vijana

0
867

Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project – JNHPP), umetoa nafasi za ajira kwa vijana wengi wa kitanzania.

Akizungumza na wadau mbalimbali leo, katika sherehe ya uchepushaji maji katika Mto Rufiji kwenye handaki, kwa ajili ya ujenzi wa tuta kuu la bwawa litalotumika kuzalisha umeme, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Zena Said amesema mradi umeajiri wafanyakazi 6,000, kati yao 5,728 ni Watanzania ikiwa ni zaidi ya 90%.

Handaki hilo lina urefu wa mita 703, upana wa mita 17 na kina cha mita 12.

Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2022.

Aidha, kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kushusha bei ya umeme na bei za bidhaa za viwandani. Vilevile kutasaidia katika kukuza uchumi wa viwanda.

Mradi huu unagharimu shilingi trlioni 6.5.