Mradi wa maji wa pili kwa ukubwa Tanzania mbioni kukamilika

0
158

Rais Samia Suluhu Hassan ametembelea mradi wa maji wa Chekereni, wilaya ya Arumeru, ambao ni mradi wa pili wa maji kwa ukubwa nchini Tanzania baada ya mradi wa maji uliopo mkoa wa Tabora

Mradi wa Chekereni unavisima 41 na tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni 3 pamoja na pampu za kusukuma maji.

Ujenzi wa mradi huo ambao maji yake siyo ya chumvi umefikia 75% na unatarajiwa kukamilika Juni 2022.

Baadhi ya wakazi watakaonufaika na mradi huo wameishukuru serikali kwani karibuni wataanza kupata maji safi na salama ambayo hayatakuwa na athari za kiafya, kama kuharibu rangi ya meno yao.

Raia Samia anaendelea na ziara yake mkoani Arusha ambapo aliwasili jana jioni akitokea mkoa wa Kilimanjaro.