Mpango waja kupima afya ya udongo

0
139

Serikali imeandaa mpango maalum wa kupima afya ya udongo ili kuwasidia Wakulima kulima mazao kutokana na ubora wa eneo, lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji.

Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde, wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho nchini kwa mwaka 2023.

Amesema kutakua na vifaa maalum vitakavyowafuata Wakulima shambani na kupima udongo ili kumwezesha mkulima kulima kilimo chenye tija.