Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, leo ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Katavi ambapo pamoja na mambo mengine anakagua miradi mbalimbali na kuzungumza na wakazi wa mkoa huo.
Katika uwanja wa ndege wa Mpanda, Dkt. Mpango amepokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Katavi pamoja na vikundi vya burudani.