Moto wateketeza bweni Chalinze

0
153

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete ametembela shule ya sekondari ya Kiwangwa, ili kujionea uharibifu uliotokea baada ya moto kuteketeza bweni la wasichana katika shule hiyo.

Akiwa shuleni hapo pamoja Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani, Hajat Mwanaasha Tumbo, wamekubaliana kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha masomo yanaendelea kama kawaida.