Mo akabidhi Bilioni 20 kwa Simba

0
191

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya soka ya Simba, Mohammed Dewji (MO), amekabidhi kitita cha Shilingi 20 ambazo ni asilimia 49 ya hisa ambazo anapewa mwekezaji katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo.

Dewji amekabidhi cheki ya pesa hiyo leo Julai 30, 2021 huku akieleza kwamba pesa aliyoiweka Simba ni zaidi ya Shilingi bilioni 20.

“Mpaka sasa nimeshaipa Simba Sh 21.3 Bilioni, ukiachana na pesa nyingine za ziada za maandalizi ya msimu, usajili na nyinginezo ninazotoa,”-amesema Mohamed Dewj

Lakini kuna watu wanasema Mohammed Dewji hana pesa, leo hii nakabidhi cheki ya Sh 20 Bilioni za hisa asilimia 49 kwa klabu ya Simba,” ameongeza mwenyekiti huyo