Mngereza kuzikwa Same Jumatano ijayo

0
498

Mwili wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza, utawasili jijini Dar es salaam Jumatatu Desemba 28, 2020.

Taarifa iliyotolewa na BASATA imeeleza kuwa, mwili wa Mngereza utaagwa Jumanne katika ukumbi wa Karimjee na mazishi yatafanyika Desemba 30, 2020 kijijini kwao Suji wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Mngereza amefariki dunia Desemba 24 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU).