Mmoja wa pacha waliotenganishwa afariki dunia

0
197

Mmoja wa pacha waliotenganishwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo mkoani Dar es Salaam (Rehema na Neema) amefariki dunia.

Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Eligaesha ameiambia TBC kwa njia ya simu kuwa watoto hao walifanikiwa kuvuka saa 72 ambazo ni hatarishi lakini walikuwa katika chumba cha uangalizi maalum( ICU).

“Ilipofika Jumapili saa tatu asubuhi mtoto mmoja ambaye ni Neema hali yake ilibadilika ghafla na madaktari wakaendelea kujitahidi kuona namna ambavyo wanaweza wakamrudisha katika hali yake ya kawaida, lakini ilishindikana”amesema Eligaesha

Amesema mtoto Rehema ambaye amebaki hali yake inaendelea vizuri na madaktari wanaendelea kutoa huduma sahihi na kwa wakati.