Mkutano wa Watafiti na Walimu wa elimu ya awali wafunguliwa

0
245

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema  kuwa,  Serikali itaendelea kuwekeza katika elimu ya awali ili kujenga msingi wa elimu kwa watoto wa Kitanzania katika ngazi ya awali hadi Vyuo Vikuu.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kufungua mkutano wa Saba  wa Watafiti na Walimu wa awali kutoka nchi Tisa za Afrika, Asia na Amerika, Profesa Ndalichako amesema kuwa, tayari Serikali imedahili zaidi ya walimu wa awali Elfu Tatu kwa mwaka huu pekee ikiwa ni jitihada za kuimarisha kiwango cha Elimu hapa nchini.

Mkutano huo wa Saba wa Watafiti na Walimu wa awali unahudhuriwa na Washiriki kutoka nchi za New Zealand, Marekani, Denmark, Kenya, Uganda, Nigeria, India, Pakistan na Mwenyeji Tanzania.