Mkutano wa Uwekezaji waendelea Sweden

0
364

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa  Palamagamba Kabudi amesema kuwa serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha wawekezaji wanakuja kuwekeza nchini.

Profesa  Kabudi ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza kwa njia ya Video na washiriki wa mkutano unaohusu fursa za uwekezaji unaoshirikisha Watanzania wanaoishi nchini Sweden.

Aidha Profesa Kabudi amewataka Watanzania hao wanaoishi nchini Sweden kuiwakilisha nchi yao kwa kufanya mambo mazuri ambayo yataijengea Tanzania taswira nzuri katika Jumuiya ya Kimataifa.

Kwa upande wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, -Job Ndugai ambaye anashiriki mkutano huo,  amewahimiza wawekezaji wa Sweden kuja kuwekeza  Tanzania katika sekta mbalimbali.