Mkutano wa SADC ni fursa kubwa ya kukuza utalii wa Tanzania: Dkt Kigwangalla

0
206

Waziri wa Maliasili na utalii  Dkt. Hamis Kigwangalla amesema mkutano wa SADC ni fursa ya kukuza sekta ya utalii, pamoja na watoa huduma kutoa huduma bora ili kukuza sekta hiyo. Akizungumza Jijini Dsm Waziri Kigwangalla amesema  kuwa watoa huduma hawana budi kutoa huduma bora zitakazokidhi mahitaji na hivyo kuweza  kupanua wigo wa fursa zitokanazo na utalii wa mikutano.

Nao Baadhi ya watoa huduma za malazi na chakula  Jijni Dar es salaam wamesema kuwa ujio wa wageni wa SADC umekua na manufaa kwao na kusema wamejiandaa kutoa huduma bora zitakazofanya wageni hao kutaka kurejea tena hapa nchini.

Gloria Michael/James Range