Mkutano Mkuu wa mwaka wa vyombo vya Utangazaji vya Umma kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) – SABA, umeanza leo mjini Livingstone nchini Zambia.
Akifungua Mkutano huo unaojumuisha Wakuu wa vyombo vya Utangazaji kutoka nchi 16 za SADC, Waziri wa Habari wa Zambia, – Dorah Siliya amesema kuwa changamoto ya vyombo vya Habari vinavyochapisha habari mtandaoni ni kubwa hasa katika kuwasilisha maudhui yenye ukweli na uhakika.
Kwa upande wao washiriki wa mkutano huo wa siku Tatu wamesema kuwa, vyombo vya Utangazaji vya Umma havina budi kuendana na wakati ili kushindana na vyombo vya Habari vinavyochapisha habari mtandaoni.
Miongoni mwa Washiriki wa mkutano huo ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayub Rioba na Arther Asiimwe ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Rwanda.

