MKUTANO WA DINI WAATHIRI MECHI YA SIMBA vs YANGA

0
168

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetangaza mabadiliko ya ratiba za michezo yote ya mzunguko wa 26 wa ligi hiyo pamoja na michezo mingine miwili.

Pamoja na kuathiri mzunguko wote, michezo miwili iliyoathiriwa na ratiba hiyo ni Geita Gold dhidi ya Coastal Union na mchezo mwingine ambao ni Simba SC dhidi ya Yanga SC.

Katika barua yao ya mabadiliko ya michezo hiyo, bodi ya ligi imesema imepokea barua kutoka kwa wamiliki wa Uwanja wa Benjamin Mkapa ikieleza kuwa tarehe 9 Aprili kutakuwa na mkutano wa dini na kufanya kusogezwa mbele kwa mchezo huo.

Kutokana na mabadiliko ya mchezo wa Aprili 9, michezo yote ya mzunguko wa 26 imeathirika.