Waziri Mkuu Kassim Majaliwa muda mfupi ujao atafungua rasmi mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), mkutano unaofanyika jijini Arusha.
Mkutano huo unawakutanisha Wakuu wa Polisi kutoka nchi 14 za Ukanda wa Mashariki mwa Afrika, kwa lengo la kujadili masuala ya usalama na kudumisha ushirikiano katika kushughulikia masuala ya uhalifu.
Wakati wa mkutano huo , Mwenyekiti wa sasa wa EAPCCO ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Sudan, -Adil Mohamed Ahmed Bashir atakabidhi Wadhifa huo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Tanzania, – Simon Sirro baada ya muda wake kumalizika