Mkutano wa 12 wa Bunge kuanza kesho

0
148

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Leo ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kilichofanyika katika ofisi za Bunge jijini Dodoma ambapo kimepokea na kujadili mapendekezo ya ratiba ya mkutano wa12 wa Bunge.

Mkutano huo wa 12 wa Bunge utakaofanyika kwa muda wa wiki mbili, utaanza kesho Agosti 29, 2023 na unategemewa kuhitimishwa Septemba 08, 2023.