Mkutano SADC fursa nzuri ya Utalii – Naibu Waziri Kanyasu

0
310

Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu amesema, Tanzania imejiandaa kuutangaza utalii wa kipekee wa Tanzania wakati wa Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika hapa nchini Mapema mwezi August.

Naibu Waziri Kanyasu amevitaja vivutio vya Kipekee vilivyopo hapa nchini kuwa ni pamojaMlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi Barani Afrika, Hifadhi ya Ngorongoro ambayo wanaishi wanyama Pori, Wanyama wa Kawaida na Mifugo na utamaduni wa Mtanzania ambao ni wa kipekee

Akizungumza na TBC Online Kanyasu amesema, licha ya kila nchi kuwa na hifadhi za wanyama lakini Tanzania ina vivutio ambavyo havipatikani kokote katika nchi hizo.

Naibu Waziri Kanyasu ameongeza kuwa, manufaa yanayopatikana katika sekta ya utalii ni makubwa licha ya muingiliano katika Ecolojia ya wanyama kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine