Mkurugenzi wa Mipango TAKUKURU afikishwa Mahakamani

0
545

Mkurugenzi wa Mipango,Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Kulthum Mansoor anayetuhumiwa kuwadhulumu viwanja wafanyakazi wa Taasisi hiyo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amethibitisha kukamatwa hapo jana kwa Mkurugenzi huyo  na kufikishwa mahakamani hii leo.

Amesema kuwa baada ya kukamatwa hapo jana, Kulthum alipelekwa katika katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kilichopo jijini Dar es salaam.

Baada ya kufikishwa mahakamani Kulthum amepelekwa rumande na kesi yake haina dhamana.