Mkurugenzi mkuu wa Global fund akutana na wadau

0
238

Mkurugenzi Mkuu wa Global Fund Peter Sunds amekutana na wadau mbalimbali wa masuala ya afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na taasisi binafsi na serikali.

Mkurugenzi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa taasisi ya Doris Mollel Foundation Doris Mollel ambaye amemuelezea namna ambavyo Doris Mollel Foundation imeweza kutekeleza mradi wa Global Fund nchini.

Ikumbukwe kuwa Disemba mwaka jana Doris Mollel Foundation @dorismollelfoundation ilipokea ufadhili wa kutekeleza mradi wa Global Fund uitwao Covid-19 Response Mechanism katika mikoa mitatu ya Shinyanga, Simiyu na Kagera kupitia Shirika la Amref @amreftz Tanzania.

Katika maeneo hayo, Doris Mollel Foundation iliendesha semina fupi kwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha juu ya umuhimu kwa kujikinga dhidi ya Maambukizi ya ugonjwa wa Malaria katika kipindi hiki cha cha mlipuko wa Uviko-19 na kuwahamasisha kuchanja chanjo za Uviko-19 na kuweza kuwafikia akina mama wajawazito na wanaonyonyesha zaidi ya 1,200.