Mkurugenzi Karatu akalia kuti kavu, apewa miezi mitatu tu

0
163

Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa muda wa miezi mitatu kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu, Karia Rajabu kukamilisha ujenzi wa hospitali ambayo fedha zake zimeshatengwa kukamilisha ujenzi wake.

“Karatu kuna hosipitali ya wiliaya ambayo imeanza kujengwa toka 2019 fedha yote imetolewa iko pale hosipitali haijakamilika,Mkurugenzi wa Karatu nakupa muda mchache sana,nakupa miezi mitatu kwa sababu fedha yote unayo sioni kwa nini hospitali haijaisha ina mwaka wa pili sasa kinachoendelea pale ni uzembe au mnavutana, nakupa mizezi mitatu nikija Karatu nikute hiyo hospitali imemalizika nije nifungue na wananchi wapate huduma,”- Rais Samia Suluhu Hassan.