Mkurugenzi Huduma za Redio TBC apokea TUZO

0
158

Mkurugenzi wa Huduma za Redio wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Aisha Dachi amepokea Tuzo za Wanawake wa mfano kwenye tasnia ya habari nchini Tanzania

Tuzo hizo zimetolewa jijini Dar es salaam kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA).