Mkoa wa Shinyanga watakiwa kuharakisha ujenzi wa Hospitali

0
1352


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kuharakisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa .

Amesema hospitali hiyo itakayosaidia serikali kuboresha huduma za afya kwa kuongeza idadi ya madaktari bingwa Mkoani Shinyanga na kuweza kukabiliana na tatizo la vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga mkoani humo.

Hata hivyo Waziri Ummy ameeleza kuwa  halmashauri ya manispaa ndiyo itakayokuwa na jukumu la kusimmamia miundombinu ya hospitali hiyo mara itakapokmalika.