Maelefu ya wananchi wa Zanzibar wakiongoza na Mgeni Rasmi Waziri wa nchi ofisi ya Rais katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman wamejitokeza katika viwanja vya Maisara kisiwani Unguja katika usiku wa Fashfash kuamkia tarehe 12 Januari Ikiwa ndio siku ya kilele cha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Usiku wa Fashfash umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya Siasa, Serikali na Sekta binfasi ikiwa ni kuunga mkono falsafa ya miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Shamrashamra za miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofikia kilele chake January 12, Yameambatana na shughuli mbalimbali yakiwemo maonesho ya biashara ya Mapinduzi.