Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa akamatwa kwa tuhuma za rushwa

0
271

Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibr (ZAECA) inamshikilia mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa kwa tuhuma za kuanza kampeni kabla ya muda na kutoa ahadi za rushwa.

Lulu Mwacha (29) ambaye ni mkazi wa Arusha amekamatwa huku ZAECA ikiendelea kufanya mahojiano na wote walioshirikiana nae.

ZAECA pia imerekebisha taarifa ya awali waliyoitoa kuhusiana na mtuhumiwa kwamba umri wake ni miaka 29, na si miaka 34 kama ilivyokuwa imeripotiwa awali.