Miundombinu ya elimu yaboreshwa Dodoma Mjini

0
113

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ameishukuru Serikali kwa kuboresha mindombinu ya elimu katika jimbo hilo.
 
Katika jimbo hilo la Dodoma Mjini, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imedhamini na kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu yenye lengo la kuweka mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia.
 
Mavunde ametoa shukrani hizo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali iliyopo kwenye jimbo hilo la Dodoma Mjini, ambapo miongoni mwa miradi hiyo ni shule ya msingi ya Medeli ambayo ilifanyiwa ukarabati na kuongezewa vyumba vipya vya madarasa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na TEA.
 
Miradi mingine aliyokagua ni ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa, matundu ya choo, ukarabati wa madarasa ya zamani pamoja na ule wa uchimbaji wa kisima cha maji uliotetekelezwa na TEA kwa gharama ya shilingi milioni 345.
 
“Ninaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuipa sekta ya elimu kipaumbele na leo tunashuhudia utekelezaji wa miradi mikubwa ya elimu, kwa furaha niliyonayo leo nitawanunulia seti  moja ya kompyuta kwa ajili ya uchapishaji wa mitihani hapa shuleni ili tuwaandae vyema watoto wetu wenye mitihani ya mwisho ya Taifa, amesema Mavunde