Baraza la Mitihani la Tanzaina (NECTA) limetoa wito kwa Kamati za Mitihani na Halmashauri zote nchini kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji wa mitihani ya Taifa zinazingatiwa ili kuzuia mianya ya udanganyifu katika mtihani wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 na 12 mwezi huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde amesema kuwa Watahiniwa 947, 221 wanatarajiwa kufanya mtihani huo Tanzania Bara.
Dkt Msonde amewataka wamiliki wa shule kutoingilia shughuli na taratibu za Wasimamizi katika kipindi chote cha mitihani hiyo na kuongeza kuwa NECTA haitasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayebainika kujihusisha kwa namna yoyote katika udanganyifu wa
mitihani hiyo.