Miti ya matunda kukuza matumizi ya nishati safi

0
269

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuongeza kasi ya kupanda miti ya matunda ambayo itasaidia kupunguza kasi ya ukataji miti nchini, kuongeza matumizi ya nishati safi na kutunza mazingira.

Rais Samia ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati akifungua Mjadala wa Nishati Safi ya Kupikia unaofanyika kwa muda wa siku mbili na kushirikisha wadau mbalimbali wa nishati.

Amesema kupanda miti hasa ya matunda kutasaidia kuondokana na ukatwaji wa miti ambayo mingi watu huona haina faida.

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuna umuhimu wa kuacha kukata miti ya asili kaajili ya kuni na mkaa na badala yake itumike kwa ajili ya ufugaji wa nyuki.