Mita za maji zinasoma upepo

0
170

Wakazi wa kijiji cha Nyangova wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma, wamedai kuwa baadhi ya mita za maji zilizofungwa kwenye maeneo yao zinasoma upepo badala ya maji.

Wakazi hao wamemueleza mkuu wa mkoa wa huo Thobias Andengenye kuwa tatizo hilo linawalazimu kulipia ankara za maji ambazo kiuhalisia wanakuwa hawajazitumia.

Akizungumza katika mkutano huo meneja wakala wa maji mijini na vijijini (RUWASA) Halmashauri ya Kigoma mhandisi Leo Respicius, amekiri kuwepo tatizo hilo na kusema kuwa linatokana ubovu wa baadhi ya mita za wateja ambapo maji yanapokuwa yamefungwa zenyewe zinaendelea kuzungunka.

Aidha amesema tayari wakala huo umeanza kushughulikia suala hilo kwa kuruhusu maji kukaa kwenye mabomba muda wote.

Kufuatia suala hilo mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameiagiza RUWASA kuhakikisha changamoto hiyo inakwisha Ili wananchi wafuraie huduma ya maji kwa gharama za matumizi halisi.

Mkuu huyo wa mkoa wa Kigoma anaendelea na ziara ya kukagua miradi ya maji mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi.