Miswada mitatu yawa sheria

Kutoka Bungeni

0
206

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia miswada mitatu kuwa sheria kamili na tayari zimeanza kutumika.

Akitoa taarifa Bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema miswada hiyo ni pamoja na muswada wa sheria ya Uwekezaji Tanzania wa mwaka 2023, Muswada wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi na muswada wa marekebisho wa sheria mbalimbali namba 3 wa mwaka 2022.

Miswada hiyo iliyopitishwa katika mkutano wa 9 wa Bunge imepatiwa kibali na Rais Samia na sasa kuwa sheria kamili.

Spika Tulia amesema miswada hiyo sasa itatambulika kama sheria ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka 2022, Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ya mwaka 2022 na sheria ya mabadiliko ya sheria mbalimbali namba 3 ya mwaka 2022.