Miradi ya Mendeleo ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

0
263

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ,mkoa wa Singida limeanzisha miradi mbalimbali ambayo imelenga kupunguza gharama za uendeshaji wa Jeshi hilo pamoja na kuongeza kipato cha askari wa jeshi hilo.


Akikagua shughuli zinazofanywa kwenye Karakana ya jeshi hilo mkoa wa Singida,Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji ,Thobias Andengenye amesema miradi hiyo itawezesha Jeshi hilo kutatua changamoto mbalimbali za uhaba wa vifaa kuongeza pato la askari wa jeshi hilo katika siku za badae.

Ufugaji wa kuku na utengenezaji wa thamani mbalimbali ni sehemu ya miradi iliyobuniwa na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Singida ambayo tayari imeanza kuingiza mapato ndani ya jeshi hilo.


Kamanda wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Singida ,Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Jeshi hilo ,Ivo Ombella amesema miradi hiyo imeanzishwa kutokana na michango ya askari wa jeshi hilo mkoa wa singida kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.


Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji ,Thobias Andengenye amekagua miradi inayofanywa na Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Singida na kueleza mtazamo wake kuhusiana na miradi hiyo

Pamoja na hilo amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano za kuimarisha utendaji kazi wa jeshi hilo la Zimamoto na uokoaji

Baadhi ya miradi inayotekelezwa na jeshi la zimamoto kwa kutumia nguvu zao ni ufundi seremala,ufundi umeme,ushonaji wa nguo mbalimbali zikiwemo za askari pamoja na mradi wa utengenezaji wa matofali na vigae.