Miradi mikubwa ya maji kukamilika Machi

0
101

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Wazri wa Maji, Jumaa Aweso kukamilisha miradi miwili mikubwa ya maji iliyopo Makuyuni mkoani Arusha ifikapo mwezi Machi mwaka 2023.

“Waziri tunakupa miezi mitatu kutoka mwezi wa 12, mwezi wa tatu mwakani wananchi hawa waanze kupata maji. Ikimpendeza Mungu kabla ya hapo tutashukuru sana. ” ameagiza Rais Samia

Rais Samia ambaye hii leo amehitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Manyara ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wakazi Makuyuni akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha.

Kwa upande wake Waziri Aweso amewaambia wakazi hao wa Makuyuni kuwa fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa maji utakaotoa lita milioni 1.1 za maji kwa siku zitapatikana na utekelezwaji wake utaanza mara moja.

Amesema mradi huo utapunguza shida ya maji si kwa wakazi wa Makuyuni pekee bali pia Monduli na vijiji vingine 13.