Miradi inayotekelezwa na Serikali imekua na manufaa kwa Wananchi : Makonda

0
132

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, – Paul Makonda amesema kuwa, miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano, imekuwa na manufaa makubwa kwa Wananchi pamoja na Taifa.

Akizungumzia miaka Minne ya Serikali ya awamu ya Tano madarakani kwa mkoa wa Dar es salaam mbele ya Viongozi mbalimbali wa Dini pamoja na wale wa Taasisi za Dini, Makonda amesema kuwa miradi hiyo ikiwemo ile ya Barabara, Afya, Maji na Elimu imeleta unafuu wa maisha ya kila siku ya Wananchi.

Makonda pia amezungumzia hali ya amani na usalama katika mkoa wa Dar es salaam, na kusema kuwa hivi sasa mkoa huo hauna matukio ya kutisha kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mbali na Viongozi wa Dini , mkutano huo pia umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam.