Miradi 38 kupitiwa na mwenge Kilimanjaro

0
125

Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Kilimanjaro ambapo utakagua, kutembelea na kuzindua miradi 38 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 13.6.

Akizungumza wakati akipokea mwenge huo kutoka mkoani Tanga,  mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai amesema miradi itakayotembelewa ni ile ya afya, elimu, maji na barabara.

Kagaigai amewataka wananchi walioko katika miradi hiyo kuitunza ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.