Mipaka ya hifadhi ya Tarangire kupitiwa

0
152

Serikali imesema itatuma wataalam wa wizara ya Maliasili na Utalii na wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia mipaka ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo.

Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja wakati akijibu swali la mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo, ambaye ametaka kujua mkakati wa serikali kumaliza migogoro ya mipaka kati ya vijiji vya Vilima vitatu, Mwada na Ngolee ambavyo vinapakana na hifadhi ya taifa ya Tarangire.

Amesema serikali inatambua uwepo wa changamoto za migogoro katika hifadhi ya taifa ya Tarangire na katika kuleta maelewano itatuma wataalam ambao wataenda kutafsiri mipaka ya wananchi ili waheshimu mipaka ya hifadhi hiyo.

Hata hivyo Naibu waziri Masanja amewataka wananchi wanaoishi karibu na mlima Kilimanjaro kuendelea kuhifadhi uoto katika maeneo yanayozunguka mlima huo.