Wizara ya Maliasili na Utalii nchini imeweka mkakati wa kuhakikisha maeneo ya Malikale yanakuwa rafiki kwa wawekezaji ili kuvutia watalii zaidi, kuinua pato la taifa pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Francis Michael alipokuwa akifungua rasmi kikao cha wadau wa Utalii na wataalam wa Malikale ili kujadili miongozo ya uwekezaji katika maeneo ya Malikale nchini.
Licha ya kuwashukuru wadau hao kwa kuitikia wito na kuudhuria kikao hicho, Dkt Michael amesema majadiliano hayo yataleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Utalii na kwa matumizi endelevu ya urithi wa Utamaduni kwa manufaa ya vizazi cha sasa na vijavyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Malikale nchini Dkt. Kristowaja Ntandu, ameleza kuwa japo utalii wa Malikale unazidi kukuwa kwa kasi, lakini wameona haja ya kukaa chini na wadau wa Utalii ili kupeana miongozo ya namna bora ya uwekezaji katika maeneo hayo ili kazi ya uhifadhi iwe endelevu.