Milioni 30 zatolewa kwa wahanga wa mafuriko Lindi.

0
273

Baadhi ya maeneo hapa nchini yamekumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha vifo, upotevu wa mali na uharibifu wa makazi yao.

Wananchi wa China nchini Tanzania kupitia taasisi ya Overseas Chinese Service Center, wamejitokeza kwa umoja na kuweza kuchangia vitu vyenye thamani ya Tsh 30 milioni kwa wahanga wa mafuriko Lindi.

Akikabidhi 2350kg za unga, nguo 5000, vitabu 1200, viatu jozi 3600, Mkurugenzi wa taasisi hiyo Alston Yi, amesema kuwa vitu hivyo vitasaidia kwa sehemu waathirika wa maafa mkoani huko.

Taasisi mbalimbali zimetakiwa kujitolea kusaidia wahanga wa maafa ya mafuriko yanayotokea hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Jonston Weston, Meneja wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa, shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) wakati akipokea msaada huo.

Weston amewatahadharisha wananchi wa Lindi kusikiliza tabiri za hali ya hewa,”ushauri wanaopewa” na kujitahidi kuzingatia usafi ili kuepuka “magonjwa ya milipuko.”

Makabidhiano hayo yamefanyika leo, Februari 17, jijini Dar es Salaam.