Mikusanyiko yazuiwa kudhibiti corona

0
205

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesitisha kwa muda shughuli zote zisizo za lazima zinazohusisha mikusanyiko pamoja na makongamano yasiyo ya lazima, ikiwa ni moja ya jtihada za mkoa huo katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Sendiga amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona maambukizi ya virusi vya corona mkoani Iringa yanaendelea kuongezeka.

Amewataka Wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona ikiwa ni pamoja na kunawa mikono.mara kwa mara kwa maji tiririka, na kuvaa barakoa wawapo katika maeneo yenye watu wengi ikiwa ni pamoja na kwenye vyombo vya usafiri.