Mikoa ya Dar es Salaam na Manyara yapata wakuu wapya wa mikoa

0
331
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza mara baada ya kumuapisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hafla imefanyika Wilayani Chato Mkoani Geita, Mei 3, 2020.

Rais John Magufuli amemteua Abubakar Kunenge kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuchukua nafasi ya Paul Makonda.

Kabla ya uteuzi huo, Kunenge alikuwa Katibu Tawala wa mkoa huo wa Dar es salaam.

Rais Magufuli pia amemteua Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa mkoa wa Manyara, ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Mkirikiti anachukua nafasi ya Alexander Mnyeti.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Rais jijini Dodoma imeongeza kuwa Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa viongozi wengine mbalimbali.