Mikataba 5 ya ujenzi wa miundombinu yasainiwa

0
135

Leo Juni 30, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam, imesainiwa mikataba minne ya ujenzi wa miundombinu ya Usafiri wa Haraka wa Mabasi (BRT) awamu ya nne kwa mkoa wa Dar es Salaam na mkataba mmoja wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.

Mikataba iliyosainiwa ni pamoja na ule wa
ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa Kilomita 13.5 kutoka Maktaba ya Taifa – Mwenge (ikijumuisha kipande cha Barabara ya Sam Nujoma) – Ubungo.

Mwingine ni ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa Kilomita 15.63 kuanzia Mwenge mpaka Tegeta na ujenzi wa Karakana (Depot) mbili na Kituo Kikuu cha mabasi kimoja.

Mikataba mingine iliyosainiwa ni pamoja na ya
uboreshaji wa miundombinu ya barabara na upanuzi wa sehemu ya barabara ya Ubungo hadi Kimara yenye urefu wa Kilomita 5 kutoka njia 6 hadi njia 8 na ujenzi barabara ya TAMCO – Vikawe- Mapinga (22km), kipande cha Pangani – Mapinga (13.59km) kwa kiwango cha lami.