Miili ya watu wawili kati ya 19 waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air iliyotokea mkoani Kagera tarehe 6 mwezi huu imewasili mkoani Arusha, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika katika maeneo tofauti mkoani humo.
Akizungumza wakati wa kupokea miili hiyo, mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amesema, mwili mmoja utazikwa katika halmashauri ya Arusha na mwingine katika halmashauri ya Meru wilayani Arumeru.
Miili hiyo iliyosafirishwa kwenda Arusha ni ya Zaituni Mohamed na Aneth Kaaya.