Miili ya watu wawili imepatikana katika ajali ya basi la Machame, iliyotokea jana katika eneo la Kiongozi nje kidogo ya mji wa Babati mkoani Manyara, na kufanya idadi ya watu waliokufa katika ajali hiyo kufikia 8.
Akizungumza na TBC Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Babati Aretas Laurent,amesema wamepokea miili ya watu wawili majira ya jioni ambayo imepatikana wakati wa zoezi la kuinua gari.
Aretas ametaja idadi ya majeruhi waliopokelewa katika Hospitali hiyo hadi jana jioni kuwa ni watu 53, wanaume 34 na wanawake19, ambapowaliopewa rufaa ni 4
Dkt. Aretas amesema wagonjwa 5 wapo katika uangalizi wa karibu na wenye majeraha madogo madogo ni wagonjwa 44.