Mifuko ya Hifadhi ya Jamii yatakiwa kuwa na matumizi mazuri.

0
1188

Rais Dkt. John Magufuli ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa na matumizi yanayoridhisha kwa kuwa baadhi ya mifuko imekuwa na matumizi yasiyofaa.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo katika mkutano na watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi na viongozi wa serikali ambapo amesema mifuko ya hifadhi imekuwa na matumizi yasiyofaa jambo ambalo husababisha mifuko hiyo kuishiwa na kushindwa kufanya kazi kwa malengo yake ya kulipa wastaafu kama inavyotakiwa.

“Kuanzia leo nataka muache kuwa na matumizi ya hovyo ambayo hayana ulazima kwenye mifuko, badala yake mjikite kwenye malengo yaliyokusudiwa”alisema Rais Magufuli.

Ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii -SSRA kuhakikisha inasimamia mifuko hiyo na kuangalia isifanye matumizi yasiyo na tija kwa mifuko.

Rais Magufuli amesema ana mfano wa mfuko wa hifadhi ya jamii unaolipa walinzi wake kiwango kikubwa cha fedha badala ya kutumia walinzi wa SUMA JKT kwa gharama nafuu jambo ambalo lingesaidia kupunguza gharama zisizo za lazima katika mifuko hiyo.

Ameitaka mifuko hiyo kuacha mara moja kufanya uwekezaji usiokuwa na tija kwa miradi ambayo haina faida ambayo badala yake ni upotevu wa fedha huku

uwekezaji huo ukifanyika bila ridhaa ya wanachama jambo ambalo linaleta manung’uniko kwa wanachama wanaochangia.