Jeshi la polisi nchini kupitia Kikosi cha Kuzua Wizi wa Mifugo (STPU) limekamata mifugo 2,225 iliyokuwa ikisafirishwa bila kufuata utaratibu na iliyoingizwa katika mapori tengefu pamoja na vyanzo vya maji.
Kamanda wa polisi kikosi cha STPU Simon Pasua amesema, mifugo hiyo imekamatwa katika operesheni iliyofanyika kunzia mwanzoni mwa mwezi huu ambapo pia watuhumiwa 48 wamekamatwa na kukutwa na makosa mbalimbali.
Ameyataja makosa hayo kuwa ni pamoja na kuingiza mifugo katika vyanzo vya maji, kusafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine bila kuwa na kibali na kuingiza mifugo kiholela katika mapori tengefu ama vyanzo vya maji.
Mifugo hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka mkoa wa Morogoro kwenda mkoa wa Ruvuma bila ya kufuata taratibu za kisheria.