Mifugo 1,400 kupigwa mnada K’njaro

0
144

Mifugo zaidi ya 1400 iliyokamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani Siha mkoani Kilimanjaro inatarajiwa kupigwa mnada Julai 18 mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Thomas Apson amesema mifugo hiyo inajumuisha ng’ombe 482, kondoo na mbuzi 963.

Apson amesema uamuzi wa kupigwa mnada kwa mifugo hiyo unafuatia  Mahakama kutoa kibali baada ya kesi ya kukamatwa kwa mifugo hiyo kupelekwa mahakamani.

Amesema licha ya wiki moja kupita tangu mifugo hiyo ikamatwe  bado wamiliki wake hawajapatikana  mpaka sasa. 

Amesema mifugo hiyo ambayo iliingia katika mashamba ya wakulima na kula mazao ikitokea wilaya ya Longido imesababisha hasara ya zaidi ya Milioni 500.

Mnamo Julai 10 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai aliagiza mifugo hiyo kupelekwa katika ranchi ya Taifa iliyoko wilayani humo huku taratibu za kisheria zikiendelea.