MIAKA 60 YA TANAPA

0
198

Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa Hifadhi za Taifa nchini –TANAPA- Dkt. ALAN KIJAZI amesema Hifadhi ya Taifa ya SERENGETI na Mamlaka ya Hifadhi ya NGORONGORO zinatarajia kuadhimisha kwa pamoja miaka 60 ya kuanzishwa kwa hifadhi hizo kwa kushirikina na wadau ili waweze kufahamu changamoto wanazokutana nazo katika sekta ya utalii nchini

Akizungumzia maandalizi ya maadhimisho hayo jijini ARUSHA, Dkt. KIJAZI amesema Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASAN anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi Katika kilele kitakachofanyika Disemba 23 katika eneo la FORT IKOMA nje kidogo ya hifadhi ya Taifa ya SERENGETI.

Matangazo hayo ya Miaka 60 ya Serengeti na Ngorongoro yatakuwa Mubashara kupitia TANZANIA SAFARI CHANNEL.