Miaka 40 ya SADC na ushiriki wa Tanzania katika Mendeleo

0
182

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), imetimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake, huku wananchama wa Jumuiya hiyo ikiwemo Tanzania wakiendelea kuhamasisha umuhimu wa Jumuiya hiyo na mambo ya msingi yanayopaswa kuenziwa.

Hapa nchini kumefanyika Kongamano la maadhimisho ya miaka 40 ya Jumuiya hiyo katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mgeni rasmi akiwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ameelezea historia ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo.

Naye Spika Mstaafu Anne Makinda akitoa mchango wake amesema, Tanzania ina mchango mkubwa katika kuendeleza jumuiya hiyo kwani Mataifa mbalimbali yanayounda SADC yamesaidiwa na Tanzania katika kupigania uhuru wa nchi zao.

Kwa upande wa mtoa mada kwenye Lugha Martha Qorro, amependekeza uwepo wa lugha moja kwa jumuiya ya SADC ili irahisishe maendeleo kwa mataifa hayo na kuendeleza mshikamano.