Mgumba : Muongoze kwa kuzingatia sheria

0
140

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amewataka Wakuu wa wilaya za mkoa huo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya Serikali.

Mgumba ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za Mbozi, Songwe, Ileje na Momba walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kushika wadhifa huo.

Pia amewataka wasimamie na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zao.