Mganga ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kunajisi mtoto

0
371

Mahakama ya Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma imemhukumu Venas Edward (48) kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnajisi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka nane.

Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi, Katoki Mwakitalu, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kosa hilo pasi na shaka.

Venas ambaye ni mganga wa kienyeji mkazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji anatuhumiwa kutenda kosa hilo wakati mama mzazi wa mtoto huyo alipompeleka (mtoto) nyumbani kwa mganga kwa ajili ya kutibiwa.

Baada ya kufika mganga alimtuma mama huyo aende dukani kununua wembe ndipo akapata nafasi ya kufanya kitendo hicho.

Baada ya kurudi nyumbani mama alisikia mtoto wake analalamika kusikia maumivu sehemu za siri, ndipo mama alipomkagua na kugundua kuwa amenajisiwa.

Mama huyo alimsihi mwanae amueleze nani aliyefanya kitendo hicho ndipo mtoto huyo alimtaja mganga.