Mfumuko wa bei upo chini ya lengo

0
107

Mfumuko wa bei nchini umeendelea kuwa ndani ya lengo la wigo wa kuwa chini ya asilimia 5.

Mwaka 2022 mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 4.3 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.7 mwaka 2021.

Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2023/2024.

Aidha, amesema mfumuko wa bei hadi mwezi Mei 2023 umebaki kama ilivyokuwa katika kipindi hicho hicho mwaka 2022 ikiwa ni wastani wa asilimia 4.0.

Hali hiyo imesababishwa na kuongezeka kwa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma na kuongezeka kwa upatikanaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini na nchi jirani kulikosababishwa na upatikanaji wa mvua katika maeneo yanayotegemea mvua.