Mfumo wa (SNR) kutoa taarifa kwa umma Zanzibar

0
186

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea taarifa za kiutendaji za mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR) kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu mfumo huo uzinduliwe Februari 27, 2021

Akiwa Ikulu Zanzibar Rais Mwinyi amezungumza na watendaji wa kitengo cha SNR Ofisi ya Rais ikulu, na kuongeza kuwa wasimamizi wa mfumo wa SNR wanapaswa kuhakikisha Maofisa wanaoshughulikia mfumo huo wanatimiza wajibu wao ipasavyo na kuwa serikali ya Zanzibar inakusudia kuuimarisha zaidi utumike kutoa taarifa kwa umma siku zijazo.

Rais Mwinyi amebainisha lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo kuwa ni kuwawezesha wananchi kuwasilisha malalamiko yao Serikalini ili kupatiwa ufumbuzi mapema

Aidha Rais Mwinyi amesema Serikali itaendelea na juhudi za kutatua changamoto za wananchi wake na hivyo akaomba kuwepo na ushirikiano kwa kila mmoja kwani kwa kipindi cha mwaka mmoja wa matumizi ya mfumo wa SNR, asilimia 73 ya malalamiko yaliyowasilishwa yamepatiwa ufumbuzi.